Pages

Pages

Monday, June 10, 2013

Sugu amlilia Ngwair kwa kuwapa vidonge vyao wasanii wa Tanzania



Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Morogoro
MBUNGE wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi, maarufu kama ‘Sugu’ amewataka wasanii wasibweteke na umaarufu wanaopata, hasa katika vifo vyao, wakati wanaishi maisha magumu.
Mbunge Sugu alipomuaga marehemu Ngwair
Sugu aliyasema hayo alipokuwa anazungumza na wakazi wa Morogoro na wageni waliokwenda kumuaga marehemu Abert Mangweha ‘Ngwair’, aliyofariki Jumanne iliyopita, nchini Afrika Kusini.

Alisema kuwa Ngwar amefariki Afrika Kusini akiwa katika mihangaiko, lakini maisha yake ni kama yaw engine, maana wamekuwa wakiishi kwa tabu, licha ya kufanya kazi nzuri na kupendwa na watu wengi.

Alisema jambo hilo ni changamoto kubwa kwao, hivyo wasanii wote lazima wajipange kuendeleza harakati kwa ajili ya maendeleo yao kwa ujumla, maana hali ya wasanii inazidi kuwa mbaya.

“Wasanii tusidanganyike na hali hii ya kujaza uwanja katika vifo vyetu, ila lazima tujuwe tatizo lipo wapi na kufanya mambo makubwa, sambamba na kuizindua serikali yetu.

“Tunaamini kwa pamoja, mambo yatakuwa mazuri, hivyo huu ni wakati sasa wa kufanya kazi huku tunajua namna gani tunaweza kujikomboa, maana umaarufu na vifo vya aina hii vyenye kujaza watu wengi ni njia ya kuonyesha namna gani vijana tunakubalika,” alisema Sugu.

Sugu ni miongoni mwa wasanii wanaokubalika mno katika tasnia ya muziki wa Hip Hop, ambaye kwa sasa anaendeleza harakati zake hata baada ya kufanikiwa kuingia Bungeni, akiwakilisha jimbo la Mbeya Mjini.

No comments:

Post a Comment