Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Kata
ya Makumbusho, leo kimefanya semina ya viongozi wa Matawi, kwa ajili ya kuwapa
mafunzo ya namna gani ya kukiendesha chama chao ili kiendelee kupendwa na
Watanzania wote.
Semina inatanguliwa na wimbo wa ufunguzi kwa nyimbo mbalimbali za kukijenga chama.Calist Lyimo akifungua semina hii kama MNEC wa wilaya ya Kinondoni mbele ya viongozi wa matawi ya Kata ya Makumbusho, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Simba wa zamani, Hassan Dalali, mwenye kofia akiwa kwenye semina hii. Kulia kwake ni Calist Lyimo, MNEC wilaya ya Kinondoni, huku kushoto kwake ni Katibu wa Kata ya Bunju, akiwa kama mtoa mada.
Viongozi wa CCM Kata ya Makumbusho wakifuatilia maelezo ya watoa mada, hawapo pichanai.
Semina ya viongozi wa matawi CCM Kata ya Makumbusho ikiendelea, huku nyuma yao ni Yusuph Mhandeni, Mchumi wa CCM Kata ya Makumbusho.
Semina hiyo ilifunguliwa rasmi
na MNEC, Calist Lyimo, wilaya ya Kinondoni, huku mtoa mada mkuu akiwa ni Katibu
wa CCM wilaya Kinondoni, Mwinyimkuu Sangaraza.
Viongozi mbalimbali wa CCM Kata
ya Makumbusho, walihudhuria semina hiyo ya kujitafakari upya, ikiwa ni kuelekea
kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka 2014.
Vitu mbalimbali vilijadiliwa
katika semina hii ambapo pia ni sehemu ya kuweka mambo sawa kwa ajili ya
kukitetea chama na kuwapatia maisha bora, kutokana na utendaji na usimamizi wa
chama.
No comments:
Post a Comment