Pages

Pages

Wednesday, June 19, 2013

Mama wa Mgombea urais mwaka 2010, Fahmi Dovutwa afariki Dunia, kuzikwa kesho Kisarawe mkoani Pwani



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MAMA wa Mgombea Urais mwaka 2010 kwa tiketi ya Chama (UPDP), Fahmi Dovutwa ambaye pia ndio Mwenyekiti wa Chama hicho, Mwazarau Salum Ally, amefariki usiku wa kuamkia leo na mazishi yake kupangwa kufanyika kesho, saa nne asubuhi, Mwanalumango Kisarawe mkoani Pwani.


                           Fahmi Dovutwa, Mwenyekiti wa UPDP
Dovutwa aligombea urais mwaka 2010 sambamba na Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wagombea wengine, akiwamo Willbroad Slaa kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.

Kaimu Katibu Mkuu wa UPDP, Felix Makuwa, alisema kuwa mazishi ya mama wa mwenyekiti wao, Dovutwa yamepangwa kufanyika kesho Kisarawe mkoani Pwani.

No comments:

Post a Comment