Pages

Pages

Monday, June 17, 2013

Diwani wa CCM Ilala, aahidi kuwasaidia wajasiriamali kupata mikopo nafuu shamba la heka 100



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
DIWANI wa viti Maalum Ilala, Eshe Sururu ameahidi kuwasaidia wajasiriamali zaidi ya 1125, kuwatafutia fursa za mikopo nafuu, na kuwatafutia shamba hekari 100 kwa ajili ya kilimo cha biashara.

Alitoa ahadi hiyo juzi, wakati akikaribishwa kuwa mlezi wa vikundi 46 vya wajasiriamali, vilivyopo chini ya Jumuia ya Kukuza Uchumi Ilala (JUKUILA).

Alifurahishwa na mikakati ya baadhi ya vikundi hivyo kwa kuwashirikisha watoto kwenye elimu ya ujasiriamali, na kutoa sh. 100,000 kwa ajili ya kufungua akaunti ya pamoja ya watoto ili iwasaidie kwenye kuwekeza fedha za kuwasomesha.

Alisema, familia nyingi katika vikundi hivyo, vina watoto waliomaliza masomo bila ya kuwa na mkakati wowote wa kimaendeleo.

"Tutafanya harambee kubwa ya kuhakikishahakuna mtoto anayekaa nyumbani, bali wote wanaendelea na masomo kwa ngazi waliyoishia.

"Hatutaki kuwa na Tanzania yenye vibaka, wavuta unga na bangi, tunaka kuijenga nchi yenye vijana waadilifu na wachapakazi, na serikali ya CCM inatekeleza hili kwa vitendo,"aliongeza.

Mwalimu anayefundisha ujasiriamali kwenye vikundi hivyo, Esther Hosea, aliwahimiza wanachama kukopa kwa ajili ya maendeleo, na kurudisha mikopo kwa wakati ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Aliwahimiza kutangaza bidhaa zao ambazo kwa asilimia kubwa wanatengeneza kwa mikono yao, kushirikiana na kuepuka majungu ili kuviimarisha vikundi vyao.

Diwani wa viti maalum Ilala, Eshe Sururu (kulia), akikabidhi msaada wa viti 100 kwa kikundi cha wajasiriamali cha Wapendwa katika sherehe ya kukubali kulea vikundi 46, vyenye wanachama 1125, iliyofanyika Dar es salaam juzi. Vikundi hivyo vipo chini ya Jumuia ya Kukuza Uchumi Ilala (JUKUILA)

No comments:

Post a Comment