Pages

Pages

Monday, June 17, 2013

Chadema yazuia wabunge wake kuingia bungeni, kauli yao yapokelewa kwa hisia tofauti



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amewapiga marufuku kuingia bungeni wabunge wote ndani ya chama chao, badala yake waelekee jijini Arusha kwa ajili ya kuomboleza vifo vya waliolipukiwa na kitu kinachohisiwa kuwa ni bomu.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
Kauli ya Mbowe ni kama kususia vikao vya Bunge la Bajeti, ambalo linaendelea mjini Dodoma, ikiwa ni siku chache baada ya mlipuko huo kutokea jijini Arusha wakati yeye mwenyewe anafunga mkutano wa kampeni za Uchaguzi wa Kata nne, ambapo sasa uchaguzi huo umepelekwa mbele hadi Juni 30 mwaka huu.

Akizungumza juu ya mgomo huo, Mbowe alisema wabunge wake kutoka Chadema, hawawezi kuingia bungeni badala yake amewaelekeza waende Arusha kwa ajili ya maombolezo ya watu wanaowaunga mkono, licha ya kulipukiwa na kitu kinachohisiwa kuwa ni bomu.

Alisema kwa sasa hawawezi kusema lolote juu ya kadhia hiyo iliyosababisa vifo vya watu wawili na wengine kadhaa kujeruhiwa, isipokuwa kuacha kuingia bungeni ili waungane na wananchi wa Arusha juu ya tukio hilo la aina yake.

“Nimewaelekeza wabunge wetu wote kutoka Chadema kuwa hakuna haja ya kuingia bungeni katika Bunge la Bajeti ili tushiriki katika maombolezo haya ya watu waliokufa baada ya mlipuko huo,” alisema Mbowe.

Kauli ya Mbowe imepokelewa kwa hisia mbili tofauati, wakiwapo wale wanaomuunga mkono kutoka Chadema na wale wanaompinga yeye na chama chake kwa madai kuwa hakuna haja ya wabunge wote kwenda Arusha na kuacha bajeti inayoweza kuwanufaisha Watanzania wote.


No comments:

Post a Comment