Pages

Pages

Thursday, June 20, 2013

CRDB wazindua huduma mpya ya ‘Fahari Huduma’ kwa njia ya mawakala



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENKI ya CRDB leo imezindua huduma ya ‘Fahari Huduma’ ya kuweka na kutuma pesa kwa njia ya wakala, badala ya kwenye matawi ya benki kama ilivyozoeleka.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, DK. Charles Kimei, akizungumzia huduma mpya ya kibenki ya Rafiki Huduma mbele ya wageni waalikwa leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.



Wasanii wa THT wakicheza katika uzinduzi huo leo asubuhi.
Akizungumza katika Uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk Charles Kimei, alisema kuwa kwa huduma hiyo, wateja wao watapata huduma karibu na wanapohitaji.


Alisema kuwa wakala wote watakaosajiliwa na benki yao, wataweza kutuma pesa, kuweka au kulipa bili zao kwa njia ya urahisi zaidi, ikiwa ni ubinifu mzuri kwa ajili ya wateja wao.





Uhondo wa THT ukiendelea.



Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, DK. Charles Kimei, akizungumzia huduma mpya ya kibenki ya Rafiki Huduma mbele ya wageni waalikwa leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.



“Ni watu wachache wanaopata fursa za kibenki, ila kwa sasa kila mtu anaweza kuhudumiwa mahala popote, maana wateja wataweza kupata huduma za kibenki kwa mawakala.

“Sisi CRDB tunaamini kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wateja wetu, ndio maana wakati wote tunakaa na kuwaza njia ya kuwahudumia kwa ufanisi wateja wetu,” alisema Kimei.

Katika uzinduzi huo, wasanii kutoka nyumba ya kulea na kukuza vipaji ya Tanzania House of Talents (THT) walifanya shoo kwa wageni waalikwa katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski.




No comments:

Post a Comment