Pages

Pages

Friday, June 28, 2013

Cheka: Nipo tayari kwa vita



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA mwenye masumbwi mazito hapa nchini, Francis Cheka, amesema yupo katika kiwango cha juu, huku akiwa na uchu wa kupambana na mabondia wakubwa zaidi duniani.
                                  Bondia Francis Cheka
Cheka huenda akacheza na bondia kutoka Marekani mwishoni mwa mwezi wa nane katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, likiwa ni kuwania Ubingwa wa Dunia.

Akizungumzia hilo, Cheka alisema kiwango chake sio cha kupigana kwenye mapambano madogo, hivyo atajisikia raha kama atavaana na wenye uwezo mkubwa, wakiwamo mabondia kutoka nchini Marekani na kwingineko.

Alisema aliambiwa kuw anatafutiwa pambano dhidi ya bondia kutoka Marekani, hivyo kiwango chake kwa sasa kinaruhusu kupigana na wanamasumbwi wa huko baada ya kuwatandika wengi kutoka nchi za Afrika Mashariki na Tanzania kwa ujumla.

“Itakuwa ni siku nzuri kama nitacheza na bondia wa Marekani na mwenye kiwango chake, kama lengo la kuendeleza ubabe wangu na kujitangaza ngazi za Kimataifa.

“Naamini kila kitu kitakuwa sawa na kwa sasa najiandaa kama kawaida yangu, ukizingatia kuwa nimejipanga ili kumpiga kila anayepita karibu yangu katika kona ya masumbwi,” alisema.

Cheka ni miongoni mwa mabondia mahiri katika masumbwi hapa nchini, huku akiweza kuibuka na ushindi kwa kila bondia aliyepambana naye na kujiweka kileleni hapa nchini.

No comments:

Post a Comment