Pages

Pages

Saturday, June 29, 2013

Barack Obama aomba kumuona Mzee Nelson Mandela

          Rais wa Marekani, Barack Obama pichani.
Rais Barack Obama wa Marekani ambaye ameshaingia nchini Afrika Kusini amesema kwamba yupo tayari kumuona Nelson Mandela ikiwa familia yake itamkubalia.

Taarifa za awali kutoka nchini humo zilisema kwamba Barack Obama hataweza kumuona kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini ambaye amelazwa hospitalini.

Taarifa za Ikulu ya Marekani zilisema kwamba kiongozi huyo suala la kumuona Mandela lipo mikononi mwa wanafamilia ya mzee huyo.
Rais wa Marekani Barack Obama alipokuwa Senegal alisema kwamba ikiwa mzee Nelson Mandela atafariki dunia ushujaa wake bado utaendelea kubakia na kukumbukwa.

Alisema kwamba ushujaa wa Madiba utabakia milele, na kwa sasa anatakiwa kuombewa , hivyo sala zinahitajika kwa kila mtu ulimwenguni.

Obama alidhibitisha wiki iliyopita kwamba bado mpango wake wakuzuru Afrika Kusini upo pale pale licha ya kusikia taarifa a kuugua kwa Mandela.

Leo Obama atatembelea gereza la Robben gereza ambalo alifungwa kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini, pia atatembelea Soweto na atatembelea sehemu mbalimbali za Cape town.

Obama atahitimisha ziara yake hiyo kwa kuzungumza na baadhi wa viongozi wa nchi na wananchi wa Afrika Kusini katika Chuo Kikuu cha Cape Town.

Historia ya matatizo ya mapafu ya Mandela ilianzia tangu alipokuwa kwenye gereza la Kisiwa cha Robben karibu na Cape Town.

Aliachiwa huru mwaka 1990 baada ya miaka 27 na akaendelea kutumikia nchi kama Rais kuanzia mwaka 1994 hadi 1999.

No comments:

Post a Comment