Pages

Pages

Thursday, June 13, 2013

Afande Sele ausifia Morogoro kusheheni vipaji


Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Morogoro
GWIJI wa muziki wa Hip Hop nchini, Selemani Msindi, maarufu kama Afande Sele, amesema mkoa wao Morogoro umepata heshima kubwa, kutokana na kukusanya wasanii wenye uwezo wa aina yake.
Afande Sele akizungumza jambo katika kumuaga marehemu Albert Mangweha Ngwair mkoani Morogoro wiki iliyopita.

Afande Sele aliyasema hayo mjini Morogoro katika mazishi ya msanii Albert Mangweha Ngwair, yaliyofanyika katika Makaburi ya Kihonda Kanisani na kujaza watu wengi na kushangaza umma wa Watanzania.

Akizungumza na Handeni Kwetu mkoani Morogoro, Afande Sele, alisema Morogoro imejaa wasanii, akiwamo Ngwair ambaye kifo chake kimetokea akiwa nje ya nchi akitafuta maisha kwa kupitia sanaa yake.

Alisema kuwa wanaamini wakazi wote wa Morogoro na Watanzania kwa ujumla wataendelea kuusapoti muziki wa Tanzania, kwa ajili ya kuwasaidia wasanii, akiwamo Ngwair ambaye kwa sasa ni marehemu.

“Tunalia kwasababu tumepoteza msanii mwenzetu, aliyekuwa na uwezo wa juu kwa namna moja ama nyingine, huku tukiamini kuwa pengo lake haliwezi kuzibwa kirahisi kutokana na umahiri wake.

“Alikuwa ni msanii mwenzetu, huku akiwa ni mkazi wa Morogoro, kwasababu maisha yake kwa kiasi kikubwa ameyatumia mkoani Moro, hivyo tutaendelea kumuombea kheri na Baraka tele,” alisema Afanden Sele.

Msanii huyo ni miongoni mwa watu wanaokubalika mno mkoani Morogoro, akiitumia vyema nafasi yake ya kujichanganya na jamii kwa kupitia tasnia ya muziki wa Hip Hop nchini.

No comments:

Post a Comment