Pages
▼
Pages
▼
Thursday, May 02, 2013
Wazee wa Ngwasuma kuzuru Mbeya na Songea
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma wanatarajia kufanya shoo katika Mikoa Ruvuma na Mbeya kuanzia leo katika Ukumbi wa High Class mjini Tunduma na kumaliza na Ukumbi wa Serengeti, uliopo mjini Songea mkoani Ruvuma.
Kikosi cha FM Academia
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa FM Academia, Kelvin Mkinga, alisema kuwa pia bendi yao itafanya shoo katika Ukumbi wa City Pub, uliopo jijini Mbeya, wakati Jumapili watatoa burudani mjini Njombe, katika Ukumbi wa Turbo.
Alisema kuwa anaamini shoo hizo zitakuwa na mvuto kiasi cha kuwapa burudani wapenzi wao watakaoingia kwa wingi kujionea burudani zao kutoka kwa Wazee wa Ngwasuma.
“Ni ziara ya wiki moja kwa wapenzi wetu wa Mbeya na Ruvuma, hivyo tunaomba waje kwa wingi kwenye kumbi hizo ili kujionea namna gani vijana wao wamejipanga na wana nguvu kubwa ya kufanya shoo.
“Hata wanamuziki wetu kwa pamoja wamekuwa na hamu kubwa ya kuwahakikisha kuwa wao ni bora na wana mvuto katika utoaji burudani, hivyo hakuna lingine zaidi ya kuwaahidi burudani za kutisha,” alisema Mkinga.
Ngwasuma ipo chini Nyosh El Saadat akishirikiana na waimbaji mbalimbali akiwapo Patchou Mwamba, Pablo Masai na wengineo waliokuwa na viwango vya hali ya juu.
No comments:
Post a Comment