Pages
▼
Pages
▼
Thursday, May 02, 2013
Extra Bongo waipania shoo ya Mango Garden kesho Ijumaa
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa bendi ya Extra Bongo, maarufu kama Wazee wa Kizigo, Ally Choki, amesema kwamba wamedhamiria kufanya shoo ya aina yake katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni kesho, ambapo pia itakuwa siku ya kuwatambulisha wanamuziki wao wawili.
Ally Choki
Vijana wa Extra Bongo wakiwa kazini
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Choki alisema Ukumbi wa Mango Garden ni kati ya zile zenye mguso wa aina yake, hivyo anaamini kufanya burudani za aina yake ni sehemu ya kuwapatia raha mashabiki wao.
Alisema mbali na kupania shoo hiyo, pia mashabiki wao watapata fursa ya kuwashuhudia wakali wao wapya watakaojiunga na Extra Bongo mwaka huu.
“Tupo imara na wenye shauku ya aina yake kwa ajili ya kuipatia mafanikio bendi yetu, hivyo naamini wadau wote watapata shoo zenye mguso Ijumaa ya Mei tatu mwaka huu.
“Tunaomba wadau waje kwa wingi katika shoo hiyo itakayotumika kuwatangaza wakali wetu, hivyo huu ni wakati wa kufanya kazi kama wendawazimu,” alisema Choki.
Mbali na shoo hiyo ya Ijumaa, pia Extra Bongo huwapa burudani wapenzi wao katika Ukumbi wa Meeda Sinza kila Jumamosi, wakati Jumapili wanafanya shoo viwanja vya Garden Breeze Magomeni.
No comments:
Post a Comment