Pages

Pages

Wednesday, May 15, 2013

Wananchi waililia serikali juu ya ubovu wa barabara ya Kilombero-Ifakara unaosababisha watu walale njiani


Hii ndio barabara kuu inayotoka Kilombero kuelekea lfaraka,Mahenge na Ulanga,eneo hili limekuwa kero kubwa kwa wasafiri wanaotumia barabra hiyo, huku wananchi wakitumia barabara kuu ya Kilombero, kuelekea maeneo ya lfaraka, Mahenge, na Ulanga, wakiilalamikia serikali ya wilaya ya kilombero kwa kushindwa kukarabati shimo kubwa lililopo barabara kuu ya Kilombero-lfaraka na kusababsiha adha kubwa kwa wananchi ambao magari yao hukwama kwenye shimo hilo na kusababisha kulala hapo usiku kucha.
Shimo hilo klubwa lililojaa maji kufuatia mvua zinazoendela kunyesha lipo kwenye barabara hiyo eneo la Kidatu kilometa chache kitoka Kilombero mjini

Baadhi ya wananchi waliohojiwa na audifacejackson blog walidai kwamba shimo hilo ni la muda mrefu na kwamba viongozi mbali mbali wanapita eneo hilo na kushuhudia bila kuchukuha hatua yoyote.

"Bila huyu jamaa mwenye trekta sijua hali ingekuaje,hata hivyo jamaa huyu anafanya kazi hii kwa muda wa mchana tu ikifika jioni anaondoka zake, jana usiku kuna abiria wa basi moja walipofika hapa wamekwama na dereva alifanya jitohadi kulivusha gari lake bila mafaniki nakuradhimika kulala hapa huku baadhi ya abiria waliokuwa na  watoto wadogo wakilalamika watoto zao kung’atwa na Mbu na kupigwa na baridi    usiku kucha hadi alfaji trekta lilipofika na kulivuta basi hilo, wananchi tutavumilia lakini iko siku uvumilivu utafika kikomo”alisema Bw Abdalaman Ismail ambaye alikuwepo eneo la tukio alishuhudia ndugu zake wakitaabika kwenye eneo hilo.
 Trekta ambalo linafanya kazi ya kuyafuta magari yanayokwama kwenye shimo hilo,likifuta roli huku mataili yote manne yakiwa juu kufuatia roli hilo kuwa na mzigo mzito
                               Basi hili likijitoa kutumbukia kwenye shimo hilo 
    Wananachi wakieleke kwenye basi lao ambalo lilikwama eneo hilo kwa muda mrefu,na kufanikiwa kuvutwa na trekta hiyo

No comments:

Post a Comment