Pages

Pages

Monday, May 06, 2013

Twalipo kuitembelea Lindi Soccer Academy


Na Mwandishi Wetu
KITUO cha kuibua na kuendeleza vipaji vya cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kambi ya Twalipo wilayani Temeke Dar es Salaam, kinatarajia kufanya ziara ya kimichezo mkoani Lindi, wakiwa ni wageni wa Lindi Soccer Academy (LSA) ya mjini humo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo mchana, Ofisa Habari wa LSA, Salum Mkandemba, alisema kituo chake kinatambua umuhimu wa ushirikiano katika michezo baina ya akademi, jambo lililowasukuma kuwaomba Twalipo kufanya ziara hiyo na wakakubali.

“Ushirikiano ni muhimu katika kukuza vipaji vya vijana. Kwa kulitambua hilo, tukaamua kukaa kama taasisi na kujiridhisha kuwa Twalipo ina chachu nyingi zinazoweza kutusukuma mbele, tukawasilisha ombi letu kwao, tunashukuru wamekubali,” alisema Mkandemba.
Alisema kuwa, Twalipo Youth Soccer Foundation (TYSF) imekubali mwaliko huo na kuahidi kikosi chake cha vijana wa chini ya miaka 17 kutua mjini Lindi Juni 13, ambapo watacheza mechi kadhaa za kirafiki kwa ajili ya kuimarisha mahusiano baina yao.

Aidha, LSA imekubali kuwaruhusu nyota wake wawili Khalid Mbaraka na Nicholas John kujiunga na Twalipo, ili kutanua wigo wa kiwango na mafanikio yao dimbani, kwani inaamini kituo hicho kitawangaza na kuowaonesha katika timu mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment