Pages

Pages

Monday, May 06, 2013

Kumekucha Arusha, 10 wanaswa mlipuko wa bomu kanisani


Na Mwandishi Wetu, Arusha
JESHI la polisi mjini hapa linawashikilia watu 10, wawili kutoka Kenya,
Waarabu na Mtanzania mmoja dereva boda boda aliyefahamika kwa jina la Victor Ambross.

Habari kutoka jijini Arusha zinasema kuwa watu hao wamekamatwa kutokana na tukio la ugaidi lililotokea Parokia ya Olasiti jijini Arusha na kupelekea vifo vya watu 3 na majeruhi 42 huku watatu wakiwa kwenye hali mbaya.

Tukio hilo limezua balaa kubwa na kuzidi kuiweka Tanzania katika wasiwasi mkubwa kutoka kwa watu ambao wanaamini Watanzania wameishi kwa upendo na ushirikiano kwa wote.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitoa onyo kali juu ya sakata hilo la mlipuko wa kitu kinachohisiwa kuwa ni bomu kwenye uzinduzi wa Kanisa hilo jijini Arusha na kuleta mshtuko.

No comments:

Post a Comment