Pages

Pages

Monday, May 20, 2013

Sugu aibua upya sakata lake na Clouds kwa kuiponda Made in Tanzania, sambamba Waziri Mkuu Pinda, huku akimsifia Lady Jay Dee

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MBUNGE wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambape pia ni Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, amevunja rasmi uswahiba na Clouds FM, baada ya kuhoji uhalali wa serikali kukubali kushiriki kwenye Made in Tanzania, mjini Dodoma, wakati wao ndio walalamikiwa na wasanii Tanzania.
Siku Sugu alipopatanishwa na Ruge Mutahaba. Kulia ni Tundu Lissu na kushoto ni Emmanuel Nchimbi.
Lady Jay Dee, Komando a.k.a ANACONDA
Maneno ya Sugu yaliambatana na kumsifia kwa kiasi kikubwa mwanadada Judith Wambura, maarufu kama Lady Jay Dee ambaye kwa sasa yupo kwenye vita ya maneno na mabosi wa Clouds FM, akiwamo Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba.

Akizungumza leo mjini Dodoma, Sugu alisema kuwa kitendo cha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kushiriki kwenye Made in Tanzania, mjini Dodoma na watu wanaolalamikiwa, ni kitendo kisichokubalika, hivyo kuna haja ya watu kujiangalia upya.

“Hii haiwezi kukubalika hata mara moja, maana serikali inapenda kukurupuka katika mambo mengi, yakiwamo haya ya malalamiko ya wasanii yanayofanywa kila siku,” alisema.

Aidha, Sugu alimaliza hutuba yake kwa kumpongeza Lady Jay Dee na kumtaka aongeze bidii katika kazi zake, hasa shoo yake anayotarajia kuifanya mwishoni mwa mwezi huu.

Kwa maneno ya Sugu leo mjini Dodoma, kuna kila dalili za kuibua upya bifu lake na Kampuni ya Clouds, ambayo ugomvi wao ulifikia tamati mwaka jana kwa kusuluhishwa.
 

No comments:

Post a Comment