Pages

Pages

Wednesday, May 22, 2013

Serikali yatilia mkazo suala la michezo mashuleni


Na Mwandishi Wetu, Dodoma
NAIBU waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Kassim Majaliwa, amesema kwamba wameamua kurudisha masuala ya michezo mashuleni, ikiwa ni njia ya kuwafanya watoto washiriki kikamilifu, sambamba na kutangaza vipaji vyao wakiwa wadogo.
Naibu Waziri TAMISEMI, Kassim Majaliwa
Majaliwa alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha walimu na wazazi juu ya masuala ya michezo mashuleni, ikiwa ni ajenda muhimu ya kuwaweka sawa wanafunzi kutambua kuwa michezo ni muhimu katika maisha yao.
Akizungumza katika mchango wake kwa Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Majaliwa alisema kuwa wanaamini kwa serikali kurudisha michezo mashuleni, itakuwa na faida kubwa kwa Watanzania wote.
 
“Natumia fursa hii kuwakumbusha walimu na wazazi juu ya kutia mkazo katika jambo hili la michezo katika shule za Tanzania, tukiamini kuwa utasaidia kwa kiasi kikubwa kutangaza pia vipaji vya watoto wetu,” alisema.
 
Aidha Majaliwa pia alitumia muda wake kuipongeza wizara ya Habari kwa kuweka sera nzuri pamoja na kufanya kazi kwa bidii katika suala la michezo na utamaduni kwa maendeleo ya Taifa.

No comments:

Post a Comment