Pages

Pages

Wednesday, May 01, 2013

Redds Miss Kibaha sasa kufanyika Mei 17 mwaka huu mjini Kibaha



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAANDAAJI wa shindano la urembo la Redds Miss Kibaha 2013 wametangaza siku ya kufanyika shindano hilo kuwa ni Mei 17 mwaka huu katika Ukumbi wa Kibaha Kontena.
                         Baadhi ya washiriki wa Miss Kibaha
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Linda Media Solution (LIMSO), ambaye pia ndio Mratibu wa shindano hilo Khadija Kalili alisema siku hiyo warembo watapanda jukwaani kuonyeshana uwezo katika tasnia ya urembo.
 
Alisema ameshauriana na wadau mbalimbali juu ya kufanyika fainali hizo za Miss Kibaha na kufikia muafaka kuwa Mei 17 ndio siku nzuri kwa ajili ya kupatikana mrembo huyo.

“Litakuwa ni shindano la aina yake huku tukiamini kuwa washiriki wote ni wenye uwezo na vipaji vya aina yake kwa ajili ya kushiki kwa mafanikio kwa mabinti hao.

“Tunaamini itakuwa ni safari nzuri kwa washiriki wote huku wasichana wote wakiendelea kujifua ili wakonge nyoyo za wapenzi wa mambo ya urembo hapa nchini,” alisema.

Baadhi ya warembo wanaotarajia kuonyeshana uwezo katika shindano hilo ni pamoja na Nzeran Kitano, Martina Kapaya, Asma Said, Maud Bernad, Flora Mlowola na Nancy James, Esther Albert, Beatrice Bahaya, Jenipher Njabiri na Rachel John.
 
Warembo hao wanaofanya mazoezi chini ya wakufunzi wao Sweet Ray na Bob Rich, watapanda jukwaani kwa udhamini wa Fredito Entertainment, CXC Africa, Michuzi Blog, Handeni Kwetu Blog, The African Stars Entertainment (ASET) na Redds Premium Cold, Image Pub na wengineo.

No comments:

Post a Comment