Ajali mbili zatokea mkoani Mbeya kunapofanyika Siku ya Wafanyakazi, Mei Mosi
LICHA ya mji wa
Mbeya leo kufanyika kilele cha Sikukuu ya Wafanyakazi duniani, Mei Mosi, mkoa
huo umekumbwa na ajali mbili na kuzua simanzi katika furaha hiyo.
Habari ambazo bado
hazijathibitishwa na Jeshi la Polisi zinasema kuwa moja ya ajali hiyo ilikuwa
ikiwapeleka walimu katika maadhimisho ya Mei Mosi, ambapo mgeni rasmi ni Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Tunaendelea
kufuatilia taarifa hizo zilizotufikia hivi punde, ambapo waandishi wetu
waliokuwapo mkoani Mbeya pamoja na kwenye sherehe hizo wanahangaikia kujua
chanzo cha ajali hizo.
No comments:
Post a Comment