Pages

Pages

Tuesday, May 14, 2013

Mabaki ya mwili wa mwanamke yakutwa porini mkoani Iringa

 Hii ni sehemu ya mwili  iliyosalia kama inavyoonekana
 Mabaki ya mwili  huo yakiwa  eneo la tukio kama yanavyoonekana
 Askari kanzu  wakiuchukua mwili  huo baada ya  kukutwa  porini
 Baadhi ya  nguo  alizokuwa nazo marehemu  huyo ambae  jina halijafahamika
 Hiki ni kitenge ambacho alikuwa amevaa mwanamke huyo
 Mashuhuda wa  tukio  hilo na askari kanzu  wakitoka  kuchukua mabaki ya mwili  huo
 Mabaki ya  mwili  wa mwanamke  huyo yakihifadhiwa katika mfuko maaalum
 Wananchi  na polisi  wakiupakia mwili  huo katika gari la polisi mchana huu
Polisi  wakiuhifadhi  mabaki ya mwili  huo chumba cha maiti  hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa
..............................................................................................................................................
Mabaki  ya mwili  wa mwanamke  mmoja ambae anakadiliwa kuwa na miaka kati ya 25 hadi 30 imekutwa  eneo la Magereza  Kata  ya Miyomboni Kitanzini katika Manispaa ya  Iringa leo.
Mabaki hayo  yamekutwa majira ya saa 6 mchana  wa  leo ikiwa imesambaratika kutokana na kuoza imekutwa  leo na maofisa  wa magereza ambao  walikuwa katika  eneo hilo na  wafungwa  wakikata  miti kwa ajili ya  kuni na kukutana na mifupa  hiyo.
Baadhi ya  mashuhuda  walidai kuwa mwanamke  huyo ambae alikuwa amevalia  suruali nyeusi ,kilemba  cha kitenge  chenye madoa makundu,njano ,meusi na meupe  pamoja na skafu yenye rangi nyeupe na nyeusi huku  pembeni kukikutwa kitenge  chake  chenye rangi mchanganyiko kama kilemba kwa maana  ya makundu,njano ,meusi na meupe.

Hata  hivyo  mashuhuda  hao  walisema  kuwa  mwanamke  huyo alipoteza maisha yake kwa zaidi ya wiki  mbili kutokana na jinsi  ulivyoharibika na kukauka kupita  kiasi .

Mazingira ya  kifo cha mwanamke  huyo yanaonyesha  kuwa ni tata  kutokana na polisi  waliofika  eneo hilo kukiri  kutokuwepo kwa taarifa  yoyote ya mtu  kupotea na kuwa  yawezekana alivamiwa ama alikufa kwa matatizo yake ama alikuwa akitoka Hospitali.

Hata  hivyo  eneo hilo ambalo mabaki hayo ya mwili yamekutwa ni eneo ambalo lipo jirani  zaidi na njia ya mkato inayotokea Ipogolo hivyo  ilikuwa ni rahisi  zaidi  watu  kuuona mwili  huo.

Mabaki ya  mwili  huo yamechukuliwa na polisi na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti Hospitali ya  rufaa ya mkoa  wa Iringa.

Kwa hisani ya www.francisgodwin.blogspot.comna www.matukiodaima.com

No comments:

Post a Comment