Pages

Pages

Monday, May 27, 2013

Kesi ya Lady Jay Dee yarushwa hadi Juni 13 mwaka huu

 
                                                   Lady Jaydee
MWANADADA Judith Wambura, maarufu kama Lady Jay Dee, amepangiwa tena kurudi katika Mahakama ya Kinondoni, Juni 13 mwaka huu.

Hii ni kwa mujibu wa msanii huyo ambaye aliingia kwenye mtandao na ku-twitter kwa ajili ya kuwahabarisha mashabiki wake wanaofuatia kesi hiyo iliyofunguliwa hivi karibuni.

Kesi hiyo ilifunguliwa na Kampuni ya Clouds Media Group, chini ya Wakurugenzi wake, Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba.

No comments:

Post a Comment