Pages

Pages

Friday, May 03, 2013

Kaseba abadilishiwa bondia, kuvaana na Rasco Simwanza


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
PAMBANO kati ya Bondia Japhet Kaseba na Joseph Magudha limeyeyuka na badala yake, Kaseba sasa atapanda ulingoni Juni nane mwaka huu kwa kuparuana na Rasco Simwanza, katika Ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa, jijini Dar es Salaam.
                                          Japhet Kaseba
Kubadilishwa kwa bondia huyo kutoka Kenya ni sehemu ya kumpatia mpinzani  mwenye kiwango cha juu Kaseba ambaye kwa sasa ameonekana kuwa na kiwango cha juu katika tasnia ya masumbwi.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kaseba alisema kuwa sasa amekubali kupigana na Simwanza kutokana na uwezo wake ulingoni ili asishuke kiwango chake katika ndondi.

Alisema awali alikuwa tayari kupigana na Magudha, lakini baadaye kiwango chake kilionekana kuwa cha kawaida, hivyo waandaaji wa pambano lake kutafuta mwingine, akiwamo Mmalawi, Simwanza.

"Lengo si kucheza ngumi za kitoto, hivyo naamini kwa kubadilishiwa pia bondia huyo kutakuwa ni sehemu yangu ya maandalizi ya kujiweka sawa, ukizingatia kwamba nataka nishinde kwa uwezo si kwasababu bondia nimemzidi kiwango na utundu wa kurusha masumbwi.

"Kwa sasa mipango yangu ni kuona nafanya vyema, ndio maana niliposikia kuwa sasa nitapigana na Mmalawi nikajisikia vizuri, ukizingatia kwamba nilijua kuwa yule Mkenya si mahiri kwenye ngumi,” alisema.

Kaseba ni miongoni mwa mabondia wenye kiwango cha juu hapa nchini, huku jina lake likitajwa kama mabondia wanaoweza kufanya lolote wanapokuwa ulingoni katika mapambano mbalimbali.

No comments:

Post a Comment