Pages

Pages

Thursday, May 16, 2013

FM Academia warejea tena Kijiji cha Makumbusho kuanzia Jumamosi hii



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya muziki wa dansi nchini ya FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma, imerudi tena katika Ukumbi wake wa zamani wa Kijiji cha Makumbusho baada ya kuacha ukumbi huo kwa kipindi cha miezi mitatu na kuwasononesha wadau wao.
                     Wazee wa Ngwasuma
Awali bendi hiyo ilikuwa ikifanya shoo katika ukumbi huo, lakini kulitokea kutoelewana na vijana hao kuamua kuacha kufanya shoo hapo, jambo ambalo kwa sasa limemalizika.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa FM Academia, Kelvin Mkinga, alisema sasa vijana wao watatoa shoo Kijiji cha Makumbusho kila Jumamosi, kama kawaida yao.

Alisema anaamini kurudi tena kwenye ukumbi huo ni sehemu ya kuwaburudisha mashabiki wao waliokuwa wakihudhuria shoo yao na kupata vitu adimu kutoka kwa vijana wao.

"Tulisimama kwa miezi kadhaa kufanya shoo zetu Kijiji cha Makumbusho, lakini sasa tumerejea na Ngwasuma wataendelea na ratiba yao ya zamani ya kila Jumamosi na kuburudika kwa pamoja.

"Utaratibu huo utaanza wiki hii kuhakikisha kuwa vijana wanafanya makamuzi ya aina yake ili kuonyesha kuwa wao ni vinara na Kijiji cha Makumbusho ni mahala pazuri kwa burudani zao,” alisema Mkinga.

Wiki iliyopita Wazee wa Ngwasuma walirejea kutoka kwenye ziara zao za mikoani walipotoa burudani za aina yake, wakianzia mkoani Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Mbeya na Ruvuma.

No comments:

Post a Comment