Pages

Pages

Thursday, May 16, 2013

B-Band kuwatoa Redds Miss Ukonga 2013



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini akiwa na bendi yake ya B-Band, Banana Zoro, anatarajiwa kutoa shoo ya aina yake katika fainali za Redds Miss Ukonga 2013, zitakazofanyika katika Ukumbi wa Wenge Club, Mei 25.


                 Baadhi ya washiriki wa Miss Ukonga 2013
Warembo hao kwa sasa wanafanya mazoezi makali katika Ukumbi wa Hill Tech, Ukonga, huku wakijifua vilivyo kuhakikisha nao wanatoa burudani za aina yake katika usiku huo wa Redds Miss Ukonga.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa shindano hilo, Chiku Chambuso, alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yanaendelea, ikiwa ni kumalizana na Banana Zoro.

Alisema anaamini shoo yao itakuwa ya aina yake katika usiku huo wa kupatikana malkia wa Ukonga mwaka 2013, wakiwa na nia moja ya kuhakikisha kuwa mambo yao yanakwenda sawa.

“Tumejiandaa vilivyo kuwapatia burudani ya aina yake kutoka kwa mabinti wetu pamoja na shoo ya Banana Zoro ambaye kwa hakika watatoa vitu vyenye mguso kwa wadau na mashabiki wao.

“Warembo wetu wote kwa pamoja wapo katika nafasi nzuri na uwezo wa kuwapatia shoo ya jukwaani katika kilele hicho kitakachomtoa malkia wa 
Redds Miss Ukonga 2013,” alisema.

Wadhamini wa shindano hilo ni Redds, Z-Entertainment, UEFA go Pub, Break Point, Salut 5, Mamushka Bar, Hilltech resolt, Kiota Jungle, Business Times, Times FM na Clouds FM.

No comments:

Post a Comment