Pages

Pages

Thursday, May 02, 2013

Boniface Wambura, Jamal Malinzi wapeta, baada ya FIFA kuutaka mchakato wa Uchaguzi TFF uanze upya



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BAADA ya kutokea vuta nikuvute kati ya wagombea wa nafasi mbalimbali za Uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kamati ya uchaguzi, wagombe waliokatwa majina yao katika mchakato huo sasa huenda wakawa na nafuu baada ya mchakato wote kuanza upya.
                                      Rais wa TFF, Leodgar Tenga
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Rais wa TFF Leodger Tenga amesema kwamba mchakato wa kuwapata viongozi hao utaanza upya Oktoba mwaka huu.

Tenga alisema kwamba uamuzi wa kuanza upya kwa zoezi la uchaguzi huo umeamuliwa na Shirikisho la Soka duniani (FIFA) na kwamba mchakato wa kuchukua fomu utatangazwa upya na wagombea wote kufanyiwa mchujo kama ilivyokuwa hapo awali.

Zoezi la Uchaguzi huo uliingia doa baada ya Kamati ya Uchaguzi kuondoa majina ya wagombea wawili, Jamal Malinzi na Michael Wambura katika kuwania nafasi walizokuwa wakipigania, huku wakionyeshwa kuungwa mkono na watu wengi.


No comments:

Post a Comment