Pages

Pages

Sunday, May 12, 2013

Bondia Mbwana Matumla alia na ukosefu wa mapromota Tanzania


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi za kulipwa hapa nchini, Mbwana Matumla, amesema mchezo wa ngumi unakwenda kwa kusua sua kutokana na ukosefu wa watu wenye mapenzi kiasi cha kuandaa mapambano mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Mbwana Matumla, Bondia wa Tanzania
Tangu alivyopigana na Mkenya David Chalanga mwishoni mwa mwaka jana, Matumla hajapata pambano lolote licha ya kuwa na uwezo wa juu katika tasnia ya masumbwi nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Matumla alisema ni wakati wa watu wenye uwezo na mapenzi kuandaa mapambano ili kukuza mchezo wa ngumi hapa nchini.

Alisema bila hivyo mchezo wa ngumi utakuwa kwa kusua sua maana wenye makali yao wanashindwa kuyaonyesha kutokana na kukosa watu wa kuingia nao ulingoni.

“Napenda mchezo wa ngumi na ni sehemu ya maisha yangu, ila Tanzania tuna uhaha wa mapromota, hivyo ni jukumu lao sasa kuhakikisha kuwa wanaingia na kuwekeza kwa kupitia mchezo huu.

“Ngumi ni moja ya vitu vyenye mguso wa aina yake, maana watu wanapenda kuucheza na hata mashabiki wanaingia kwa wingi kunapokuwa na mapambano ya mabondia mbalimbali,” alisema Matumla.

Matumla ni miongoni mwa mabondia wanaofanya vizuri katika mchezo wa masumbwi, huku akinolewa na mkongwe Hamis Kinyogoli aliyewahi kuwika pia katika mchezo huo ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment