Pages

Pages

Tuesday, April 09, 2013

Wanaotaka urembo waombwa kuchangamkia shindano la Miss Kibaha 2013



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MABINTI wanaopenda kushiriki mambo ya urembo wameombwa kujitokeza kwa wingi kushiriki shindano ya la kumsaka Redds Miss Kibaha 2013.
 
Akizungumza leo mchana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa shindano hilo, Khadija Kalili alisema hadi sasa washiriki wachache wamejitokeza na kutoa fursa ya wasichana wengine kuchukua fomu za usajili ili washiriki kwenye shindano hilo.
Mratibu wa Miss Kibaha 2013, Khadija Kalili.
Alisema siku rasmi ya uzinduzi wa shindano hilo itatangazwa baadaye ambapo pia washirki hao wataanza mazoezi rasmi ikiwa ni pamoja na kutangaza pia namna ya kupatikana mrembo mwenye sifa kwa Kibaha nzima.
 
“Miss Kibaha 2013 inaandaliwa na Kampuni ya Linda Media Solution (LIMSO), ambapo pia shindano hilo litafanyika katika ukumbi wa Kontena Kibaha Maili moja.
 
“Natoa wito kwa wasichana wenye sifa na wanaotaka kutimiza njozi zao kujitokeza kushiriki  huku tukizingatia umri kati ya miaka 18 hadi 24 wenye uraia wa Tanzania hiyo ikiwa ni katika hatua ya awali ya  kumpata Miss Tanzania wa mwaka huu kwani warembo wote wa Taifa hupatikana katika hatua za  mashindano ya awali.

Mbali ya kuomba warembo kujitokeza pia Kalili ameomba wadhamini  mbalimbali  kujitokeza na kutoa sapoti ili kuweza kufanikisha shindano hilo linalofanyika mara moja tu kwa mwaka.

No comments:

Post a Comment