Pages

Pages

Wednesday, April 10, 2013

Picha zaidi za Rais Kikwete kuapishwa Uhuru Kenyatta nchini Kenya

Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Rais Mpya wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta huko Ikulu mara baada ya kuapishwa rasmi kuwa rais wa nne wa nchi hyo katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa kimataifa wa michezo wa Moi-Kasarani jijini Nairobi tarehe 9.4.2013.
Rais Mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiwashukuru Marais na wakuu wa nchi waliohudhuria sherehe za kumwapisha wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoiandaa huko ikulu jijini Nairobi.
Rais wa Kenya aliyemaliza muda wake, Mwai Kibaki akifanya mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma huko Ikulu mara baada ya sherehe ya kumuapisha rais mpya wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kukamilika.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na wake wa viongozi wa juu wa Kenya, Mama Magrate Kenyatta (kushoto) ambaye ni mke wa Rais Uhuru na Mama Recheal Ruto (kulia) Mke wa Naibu Rais wa nchi hiyo Mheshimiwa William Ruto huko ikulu jijini Nairobi mara tu baada ya kuapishwa viongozi hao tarehe 9.4.2013.
Rais wa Kenya aliyemaliza muda wake, Mheshimiwa Mwai Kibaki akifanya mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma huko Ikulu mara baada ya sherehe ya kumuapisha rais mpya wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kukamilika.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mama Magrate Kenyatta katika ikulu ya Kenya jijini Nairobi mara baada ya sherehe za kuwaapisha kukamilika. PICHA ZOTE NA JOHN LUKUWI, Nairobi, Kenya.

No comments:

Post a Comment