Pages

Pages

Wednesday, April 17, 2013

Bi Kidude afariki Dunia leo mjini Zanzibar, aliza wengi


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI nguli wa muziki wa taarabu na mkongwe kuliko wote, Fatuma Binti Baraka Bi Kidude amefariki Dunia leo mjini Zanzibar.
                      Bi Kidude


                                                 Bi Kidude


Bi Kidude akiimba
Akizungumza na Handeni Kwetu Blog, mdau wa muziki nchini, Said Mdoe, alisema kuwa marehemu Bi Kidude alifia nyumbani kwa mtoto wa kaka yake, eneo la Bububu ambapo sasa mwili wake unaandaliwa kupelekwa nyumbani kwake.
Mdau wa muziki nchini, Said Mdoe kushoto akiteta jambo na msanii wa taarabu Esha Mashauzi jike la Simba.

Kifo cha Bi Kidude kimetokea wakati watu walishawahi kumzushia mara kadhaa, ambapo baadaye mwenyewe alikanusha. Hata hivyo, Bi Kidude alikuwa akisumbuliwa mara kadhaa na maradhi ukiwapo uzee uliokuwa ukimsumbua.

Mwishoni mwa mwaka jana, Bibi Kidude alikuwa akijaribu kuwalilia wadau juu ya afya yake, huku habari ambazo baadaye ziliyeyuka zilikuwa ni kuandaliwa kwa tamasha kubwa la kumuaga msanii huyo katika muziki wa jukwaani kutokana na umri wake kuwa mkubwa.

Taratibu za mazishi ya Bi Kidude zinaandaliwa na familia yake na kila kitakachokuwa kikiendelea kitaletwa kwako kama sehemu ya kumuaga msanii huyo mkongwe na ambaye kifo chake kitagonga vichwa vya watu wengi.

No comments:

Post a Comment