Pages

Pages

Saturday, March 09, 2013

Wasanii wamtaka Rais Kikwete azime muziki kwa siku mbili


Diamond, mkali wa Bongo Fleva.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Muziki hapa nchini, limesema lipo kwenye mipango ya kufikisha ombi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ili atowe amri ya kuzimwa muziki kwa siku mbili, kama ishara ya kuonyesha kuwa wanaibiwa kazi zao, pamoja na kutoa elimu kwa jamii iheshimu zaidi kazi za wasanii wao nchini.


Hayo yamesemwa jana na Rais wa Shirikisho hilo, Ado November, katika kikao chake na viongozi wa mashirikisho mbalimbali ya muziki, katika kujadili pia ujio wa Kampuni ya kusambaza kazi za muziki duniani, kwa kupitia Kampuni ya Afrisori.

Akizungumza katika kikao hicho, November alisema, wanaamini Rais atasikia kilio chao na kuagiza mamlaka zake zote kuhakikisha kuwa shughuli zozote haziendelei na kupiga muziki, jambo ambalo litakuwa njia ya kutatua changamoto za wasanii.

Alisema ingawa ni suala gumu mno jamii kuwa mbali na muziki, hivyo jambo hilo litakuwa somo kuwa muziki ni mzuri, ikiwa ni njia muafaka ya wadau wote kupangana katika kusimamia na kuweka mkakati imara kwa faida ya wasanii wote.

“Huku kuzima muziki kwa siku mbili ni juhudi za kuashiria kuwa wasanii wamechoka dhulma wanazofanyiwa na wafanyabiashara wa Tanzania, hivyo wataelewa kila kinachoendelea.

“Naamini mambo yatakuwa mazuri kwa kukutana pamoja na Rais, ukizingatia kuwa mara kwa mara tumekuwa tukifanya naye mazungumzo ambayo kwa hakika, mengi yamekuwa na majibu muafaka kwa wasanii pamoja na kiongozi huyo wa juu wa serikali.

Aidha, November amesema ndani ya mwezi huu watatembelewa na uongozi wa juu wa Kampuni ya Africori ya nchini Uingereza inayohusika na uuzaji wa kazi za wasanii kwa kupitia mitandao, ikiwa ni njia ya juu zaidi ya kuwanufaisha wasanii Tanzania kama wanavyoendelea wengine duniani, ikihusika na masuala yote ya muziki wa mitandao.

No comments:

Post a Comment