Pages

Pages

Friday, March 08, 2013

Rais Kikwete atatua tena sakata la wasanii




Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amekubali kuwaagiza watendaji wa Shirika la Posta Tanzania, kuhakikisha kuwa wanatatua kero ya usambazaji wa kazi za wasanii pamoja na kupatikana kwa stika za kukomesha wizi huo.


Hayo yamesemwa na Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Ado November, alipokuwa akizungumza katika kikao cha viongozi wa Mashirikisho mbalimbali ya wasanii, katika hali ya kutafuta namna ya kukabiriana na kero sugu za wizi wa kazi za wasanii.

“Tunashukuru kuwa mambo yakienda sawa, Posta watahusika katika usambazaji wa kazi za wasanii, ukizingatia kuwa wao wapo nchi nzima, badala ya kuwaachia wafanyabiashara wachache.

“Kuna Watanzania wanataka kununua kazi za wasanii, lakini wanakosa kazi hizo, hivyo kujikuta nao wakiingia katika wizi kwa kuchoma katika vibanda vya wauzaji wasiokuwa na leseni za biashara hizo,” alisema.

Aidha, ujumbe kutoka Kampuni ya Africori inayohusika na masuala ya uuzaji wa kazi za wasanii na usambazaji kwenye mitandao unatarajiwa kuwasili kwa kufanya mazungumzo na wasanii mbalimbali ili kuingia nao makubaliano ya kibiashara  mapema mwezi huu.

No comments:

Post a Comment