Pages

Pages

Wednesday, March 20, 2013

Wakali kibao wa Injili kushiriki tamasha la Tumaini Jipya Machi 31 mkoani Morogoro

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMPUNI ya QS Entertainment, imeandaa tamasha kubwa la ‘Tumaini Jipya’ linalotarajiwa kufanyika Machi 31 kwenye Uwanja wa Jamhuri  mjini Morogoro likihusisha waimbaji mbalimbali hapa nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya QS Entertainment, Joseph Mhonda alisema kuwa tamasha hilo lina lengo la kuwasaidia watu wenye mahitaji  maalumu kwenye jamii ikiwemo watoto yatima na kutarajiwa pia kufanyika katika mikoa mbalimbali baada ya kuzinduliwa mkoani Morogoro likiwa na lengo kubwa la kueneza neno la bwana na mambo mengine ya kijamii katika kila mkoa watakapokuwapo.
Martha Mwaipaja akizungumza jambo na mwimbaji mwingine wa muziki wa Injili, Stara Thomas, aliyewahi kuwika pia kwenye muziki wa Kidunia, maarufu kama Bongo Fleva. 

=
 
 Martha Mwaipaja, akizungumza jambo.

 Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Joseph Mhonda, ambao ndio waandaaji wa tamasha akiwa mbele ya kamera ya Handeni Kwetu Blog.



 Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Joseph Mhonda, katikati akizungumzia uzinduzi wa tamasha hilo la Tumaini Jipya.


 Stara Thomas akiwa na wakali wengine wa muziki wa Injili Tanzania.
 Mwimbaji wa muziki wa Injili, Stara Thomas, akisikiliza kwa umakini utambulisho wa tamasha la Tumaini Jipya linalotarajiwa kufanyika Machi 31, katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, huku likiandaliwa na Kampuni ya QS Mhonda J Entertainment.

No comments:

Post a Comment