Pages

Pages

Tuesday, March 19, 2013

Wadhamini waombwa kudhamini Ruaha Marathon


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAANDAAJI wa mbio za Ruaha Marathon zinazopangwa kufanyika mwezi Mei 25 mwaka huu mkoani Iringa, wamewataka wadau na makampuni kujitokeza kudhamini kwenye shindano hilo lenye mguso wa aina yake.

Maandalizi ya mashindano hayo ya riadha yanaendelea, huku yakiwa na lengo kubwa la kuuletea tija mchezo huo pamoja na kutangaza vivutio vya utalii kwa kushirikisha watu mbalimbali duniani.

Akizungumza kna Handeni Kwetu, Mratibu wa mashindano hayo ya Riadha Marathon, Albert Sanga, alisema kwamba wadhamini wakijitokeza katika patashika hiyo, wana nafasi kubwa kushiriki njia za mafanikio kwa kujitangaza ndani na nje ya nchi.

Alisema wakati huu wanaendelea na maandalizi yao ya kuhakikisha kuwa mashindano hayo yanakuwa na mguso wa aina yake, wanaamini wadau wataungana kwa lengo hilo.

“Sisi kama waandaaji wa mashindano ya Ruaha Marathon, tupo sawa kuhakikisha kuwa tunafanikisha mbio hizi kwa mafanikio makubwa, hivyo ni jukumu lao wadhamini kutuunga mkono kama wana lengo hilo.

“Mbio hizi zitashirikisha watu mbalimbali kutoka Mataifa makubwa, kama vile Uingereza, Marekani na kwingineko, huku tukiamini kuwa kwa pamoja tutafanikisha kutangaza utalii wa ndani kwa kupitia michezo,” alisema Sanga.

Riadha ya Ruaha Marathon ni miongoni mwa matukio makubwa mkoani Iringa, huku maandalizi yake yazidi kupamba moto kwa nia ya kuliweka juu tukio hilo la aina yake na kuwaunganisha pamoja kutoka ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment