Pages

Pages

Tuesday, March 19, 2013

Extra Bongo kufanya bonge la Birthday Party



Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BENDI ya Extra Bongo inatarajia kufanya sherehe ya kutimiza miaka
mitatu tangu ifufuliwe upya ambayo iungizaji sokoni wa albamu ya pili
ya bendi hiyo iitwayo Mtenda Akitendewa.

Hayo yalisemwa na mkurugenzi wa bendi hiyo Ally Choki na kufafanua
kuwa sherehe hizo zitafanyika mara baada ya kumaliza kjushuti video za
nyimbo za Mama Shuu na Bakutuka ambazo ziko kwenye albamu hiyo.


"Tumechelewa kushuti video hizo kutokana na kutingwa na shughuli
nyingi, lakini nina uhakika siku chache zijazo tutafanya kazi hiyo na
kisha zitafuatia sherehe hizo," alisema Choki.

Choki alifafanua kuwa awali sherehe hizo zilipangwa kufanyika Oktoba
mwaka jana, lakini hazikufanyika kutokana na sababu ambazo ziko juu ya
uwezo wao ambapo sasa zitafanyika wiki chache zijazo.
 
Mipango yetu yhote ya sherehe yetu itaanza mara baada kushiriki
onyesho la Media Day ambalo Extra Bonho imealikwa burudani kwa
waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari," alisema.
 
Bendi ya Extra Bongo imekuwa ikitamba na albamu mbili za Mjini Mipango
na Mtenda Akitendewa, ambapo pia imekamilisha nyimbo mbili mpya kwa
ajili ya albamu ya tatu ambazo ni Mgeni na Awadh.

No comments:

Post a Comment