Pages

Pages

Friday, March 01, 2013

TBL yakabidhi magodoro 210 na vyandarua 200 kwa Hospitali za Kiaseni na Huruma
Kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dk Ibrahim Msengi akikabidhi msaada wa magodoro kwa mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dk Mtumwa Mwako mara baada ya kukabidhiwa na kampuni ya Bia Tanzania TBL.katikati ni mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindi.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindi,(katikati)akimkabidhi kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dk Ibrahim Msengi  msaada wa magodoro kwa ajili ya hosptali ya Huruma ya wilayani Rombo pamoja na kituo cha Afya cha Uru Kiaseni ,kulia kwake ni mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dk Mtumwa Mwako.  Jumla ya magodoro 210 na vyandarua 200 vimetolewa na TBL kwa ajili ya kituo chaAfya cha Uru Kiaseni na hosptali ya Huruma .
Wakiwa katika picha ya pamoja na Waganga wa vituo hivyo.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindi,(katikati)wakifurahia jambo na kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dk Ibrahm Msengi (Kulia )pamoja na mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dk Mtumwa Mwako mara baada yaTBL  kukabidhi msaada wa magodoro 210 na vyandarua 200 kwa kituo cha Afya cha Uru Kiaseni na hosptali ya Uhuruma .
Mganga wa kituo cha Afya cha Rau Kiaseni  Dk. Delfina Materu(katikati)akizungumza na wanahabari (hawako pichani)mara baada ya kupokea msaada wa Magodoro kutoka kampuni ya bia Tanzania(TBL)shoto kwake ni Meneja mauzo wa TBL mkoa wa Kilimanjaro Leiya Hermenegild.

No comments:

Post a Comment