Pages

Pages

Friday, March 22, 2013

Siri yavuja: Yadaiwa sanaa ina zalisha mashoga wengi


Kutokana sababu za kimaadili, habari hii imeshindwa kwenda na picha za wasanii kwa kukwepa kunyooshewa vidole kutoka kwa wadau, badala yake tumeweka picha ya kijana huyu anayedaiwa kujihusisha na vitendo vya ushoga kama alivyokutwa kwenye mtandao.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
HABARI zilizovuja kutoka kwa wadau wa sanaa, ikiwamo ya uigizaji pamoja na uimbaji wa muziki ukiwamo wa Bongo Fleva na ule wa dansi, unazalisha mashoga lukuki.

Hayo yamebainika juzi kutoka kwa mkongwe wa muziki wa dansi nchini, ambaye hata hivyo hakutaka kutajwa majina yake kwasababu za kulinda heshima yake mtaani.

Mdau huyo alisema kitendo hicho kinasababisha heshima kwa baadhi yao ya kushuka, jambo ambalo kwa kiasi Fulani linaiweka sanaa kwenye mtikisiko wa aina yake.

“Ushoga ni tabia chafu isiyostahili kuigwa hata kidogo, hivyo nikiwa kama mdau wa sanaa hakika jambo hili lilianza zamani, kiasi kwamba wengine ukiambiwa wanafanya uchafu huo utashangaa.

“Nashauri wale wote wenye tabia hii waache maana najua ni wengi katika hali ya kulinda heshima katika sanaa,” alisema mdau huyo ambaye jina lake ni kubwa katika sanaa nchini.

Hata hivyo, vitendo vya ushoga awali vilidaiwa kutawala sana kwenye soko la muziki wa taarabu, kitu kinachosababisha shoo zao nyingi kuingiza watu wa aina hiyo.

Lakini katika siku za hivi karibuni, hata shoo za muziki wa dansi, zimekuwa zikiingiza mashoga wengi, ikiwamo ile ya The African Stars Twanga Pepeta, inayofanyika kila Jumapili katika Viwanja vya Leaders Club, ambapo watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja huonekana wakipita huku na kule kuuza sura.

No comments:

Post a Comment