Pages

Pages

Wednesday, March 27, 2013

Simba, Kagera Sugar hapatoshi leo Uwanja wa Kaitaba

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MABINGWA watetezi wa Ligi ya Tanzania Bara, Simba SC, leo ingia uwanjani kumenyana na timu ya Kagera Sugar, katika Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba katika mchezo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki mkoani Kagera.
Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga
Mbali na timu ya Simba kumenyana na Kagera Sugar, mechi nyingine inayochezwa leo ni kati ya Azam na Prisons ya Mbeya, itakayopigwa katika Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamaz.


Simba wanaingia uwanjani huku wakiwa na uchu wa kushinda ili wasiendelee kujiondoa katika kushika nafasi mbili za juu, huku Ligi hiyo ikiongozwa na timu ya Yanga ikiwa kileleni kwa pointi 48, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 37.

Mabingwa hao watetezi, Simba, wameondoka  jijini Dar es Salaam kwa mafungu, baada ya wachezaji wake wanaopiga kwenye timu zao za Taifa kufuata nyuma baada ya kumaliza kwa mechi zao.

Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa wamewaomba washabiki na wanachama wote kuvunja makundi yao na kuangalia mechi hizo zilizosalia kwa ajili ya kuisaidia klabu yao.

Kamwaga alisema lengo lao kubwa ni kushinda mbele ya Kagera Sugar ili wanyakuwe pointi tatu na kufikisha 37 na kujiweka katika nafasi nzuri katika muendelezo wa ligi hiyo.

“Tunaomba wanachama na mashabiki wa Simba kuendelea kuwa kitu kimoja juu ya mechi hizi, ukizingatia ni michezo migumu iliyobaki kwa ajili ya kuhakikisha kuwa hatubaki nyuma zaidi,” alisema Kamwaga.

Aidha, katika mchezo awa Azam na Prisons ya Mbeya, mashabiki watakuwa na shauku ya kuona timu hiyo iliyoanzishwa kwa malengo makubwa, Azam inavuna nini kutokana na soka lake la uhakika inaloonyesha.

Azam watakuwa na hamu kubwa ya kushinda katika mechi yao ya leo, ili ifikishe pointi 40 na kujiweka katika  nafasi nzuri ya kuliwania taji hilo linaloshikiliwa na Simba.

No comments:

Post a Comment