Pages

Pages

Wednesday, March 27, 2013

Ngwasuma kukamua Arcade House kesho


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya muziki wa dansi nchini ya FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma, kesho Alhamis inatarajia kufanya shoo ya aina yake katika Ukumbi wa The Arcade House, Mikocheni.
Baadhi ya wakali wa FM Academia wakionekana pichani.
Shoo hiyo itakuwa na msisimko wa aina yake kutokana na wanamuziki wa bendi hiyo kupanga vitu vya aina yake kwa ajili ya kuwapa ladha za burudani wapenzi wao wanaoendelea kuwaunga mkono.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa bendi hiyo, Kelvin Mkinga, alisema kwamba shoo hiyo itafuatiwa na onyesho la Ukumbi wa Kilimani House, mjini Dodoma, Ijumaa, wakati Jumamosi watakuwapo Lufina Night Club, Tabata.

Alisema shoo zote hizo zimepangwa kuwaacha mashabiki wao hoi kwa ajili ya kuwapatia burudani za aina yake, huku akiamini kuwa kila kitu kitakuwa sawa sawa kwa makamuzi ya Ngwasuma.

“Zitakuwa ni burudani za aina yake, huku nikiamini kuwa wadau na mashabiki wetu watafurahia makamuzi ya vijana wao, ukizingatia kuwa bendi yetu ipo imara na inapendwa na kila mtu.

“Naomba mashabiki wetu waje kwa wingi katika maonyesho yetu kwa ajili ya kufurahia burudani za aina yake kutoka kwa Wazee wa Ngwasuma, bendi inayotesa katika ramani ya muziki wa dansi,” alisema.

Ngwasuma ipo chini ya Rais wa Vijana, Nyosh El Sadaat, akiwa na wanamuziki wenye uwezo wa kutisha, akiwamo Patchou Mwamba, ambaye pia anatamba katika ulingo wa filamu nchini na wengineo.

No comments:

Post a Comment