Pages

Pages

Friday, March 15, 2013

Mwisho wa kuchukua fomu CHANETA leo, wadau waombwa kujitokeza

Katibu Mkuu wa CHANETA, Rose Mkisi

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Netiboli Tanzania, Rose Mkisi, amewataka wadau wa michezo kujitokeza kwa wingi leo kuchukua fomu mbalimbali kwa ajili ya kugombea katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Machi 24, mjini Dodoma.

Wakati Rose akiyasema hayo, leo saa tija alasiri ndio mwisho wa kuchukua fomu za uchaguzi huo, huku nafasi ya uenyekiti ikiwa imeombwa na mtu mmoja tu, ambaye ni Anna Kibira.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Rose alisema nafasi kama ya mwenyekiti hadi jana jioni ilikuwa imeombwa na mtu mmoja tu, hivyo kuonyesha kuwa vado kuna umuhimu wa wanamichezo kujitokeza katika nafasi mbalimbali.

Alisema kuwa wadau wamekuwa wazito kujitokeza katika kugombea nafasi hizo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanafanya kazi ya maana kuendeleza mchezo wa netiboli hapa nchini.

“Naomba wadau na wanamichezo wajitokeze leo hadi kesho saa tija kwa ajili ya kuomba nafasi za uongozi wa CHANETA kwa kuendeleza mazuri yaliyopatikana katika kipindi kilichopita.

“Ingawa muda unaelekea mwishoni, lakini mtu anaweza kuchukua fomu hapo hapo pamoja na kuirudisha, ukizingatia kuwa hadi sasa wamejitokeza watu 11 tu kwa kuwania nafasi za uongozi CHANETA,” alisema Mkisi.

Uchaguzi huo umepangwa kufanyika mkoani Dodoma mwishoni mwa mwezi huu, huku mwenyekiti anayemaliza muda wake, Anna Bayi, akidaiwa kuwa hatatetea tena nafasi yake kwa nia ya kuwapisha wengine waongoze, hasa kama hadi leo jioni hatajitokeza katika kuchukua fomu hizo.

No comments:

Post a Comment