Pages

Pages

Tuesday, March 12, 2013

Mkuu wa wilaya Korogwe apiga mkwara mzito

Mrisho Gambo, Mkuu wa Wilaya Korogwe

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKUU wa Wilaya Korogwe, Mrisho Gambo, amesema hawawezi kuchekea vitendo vya ushirikina vinavyofanywa na baadhi ya wananchi wilayani kwake, kwa kuita waganga, kutoa uchawi bila mpango.


Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Gambo alisema vitendo vya ushirikina havina nafasi, maana wanaofanya hivyo ni wale waliokata tamaa na maisha, kwa kuona kuna wanaowatia umasikini.

Gambo alisema serikali haiamini ushirikina kama isivyoamini dini kutoka kwa wananchi wake, hivyo lambalamba anayefanya kazi zake bila mpango, anastahili kufikishwa mahakamani.

“Kuna walioita waganga bila mpang0, lakini ikumbukwe kuwa serikali haina dini wala haina imani za ushirikina, hivyo yoyote anayefanya mambo kinyume atafikishwa mahakamani.

“Hatutaki mambo hayo ya ushirikina katika utendaji wetu wa serikali, maana mara kwa mara waganga hao huchochea vurugu na kuwafanya watu washindwe kuishi kwa ushirikiano,” alisema Gambo.

Maneno ya Gambo yamekuja siku moja baada ya wilayani kwake kutokea vurugu kubwa, wananchi wakilazimisha kuachiwa kwa waganga waliokuwa wakitoa uchawi kushikiliwa na polisi.

No comments:

Post a Comment