Pages

Pages

Monday, March 18, 2013

Mchumi wa CCM aanza kulibeba tawi la Green Stone



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KADA na Mchumi wa CCM Kata ya Makumbusho, Yusuph Shaban Mhandeni, maarufu kama Yusuphed Mhandeni, jana aligawa kadi za uanachama wa klabu ya Yanga, kwa tawi la Green Stone, Mwananyamala, ikiwa ni baada ya kutolewa Makao Makuu ya klabu ya Yanga.

Makabidhiano hayo ambayo yalifanyika kwenye tawi lao, yaligubikwa na shangwe, huku miongoni mwa waliopewa kadi hizo, akiwa ni nguli wa muziki wa taarabu nchini, Malkia Khadija Omari Kopa.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam kwenye makabidhiano hayo, Yusuphed Mhandeni, alisema kuwa atafanya kila analoweza kuhakikisha kuwa tawi hilo linakuwa kubwa ili wanachama hao waweze kushirikiana kwa karibu na uongozi w Yanga uliopo madarakani kwa maendeleo ya klabu yao.

Alisema awali alifurahia kusikia kuanzishwa kwa tawi hilo, hivyo lengo lake ni kuwaunganisha wananchi wakiwamo wapenzi na wanachama wa Yanga na kufahamu njia nzuri za kuiwezesha Yanga.
 Yusuph Shaban Mhandeni, Yusuphed Mhandeni, akimpa kadi yake mwanachama wa Yanga, Tawi la Green Stone, anayejulikana kwa jina la Abdul Sengwila, jijini Dar es Salaam jana. Endelea kuisoma habari hii hapo chini.





 Waliokabidhiwa kadi wakizionyesha kwa na furaha tele.
 Yusuphed Mhandeni wa tatu kutoka kushoto waliosimama mstari wa nyuma, akiwa na wanachama wa Yanga kwa kupitia tawi la Green Stone, Mwananyamala, huku wakiongozwa na mwenyekiti wao wa tawi hilo, Lumolwe Matovolwa, maarufu kama Big ambaye pia ni msanii maarufu wa filamu hapa nchini.



"Nashangaa watu wenye mapenzi mema na michezo wapo wengi, lakini wapo kimya, hivyo naapa kushirikiana na nyinyi kwa kila hatua, ikiwapo kuwalipia kuwanunulia kadi watu ambao hawatakuwa na uwezo huo, hasa wazee watano tutakaowathibitisha ili tuwe nao.

"Mbali na kuwalipia kadi hizo, pia nitashirikiana na viongozi waliopo hapa kwa kila jambo, ikiwapo pia kugharamia safari moja ya mkoani kabla ya ligi kumalizika kama wanavyofanya wengine kwa ajili ya Yanga,” alisema Mhandeni.

Green Stone lilianzishwa rasmi mapema mwaka huu likiwa chini ya viongozi wa muda, Mwenyekiti ni Lumolwe Matovolwa maarufu kama ‘Big’ na Katibu wake ni Ally Regani, ambao kwa mara ya kwanza wamepewa kadi tano Makao Makuu ya Yanga kwa ajili ya kuwapa wanachama wao.

Watu ambao wamekabidhiwa kadi hizo na Mhandeni ambaye ni kama mlezi wa tawi hilo ni pamoja na Filbert Mbezi Simon, Abdu Sengwila, Rajabu Mbwana, Joseph Joseph Chilumba, Anthon Amulike na Khadija Kopa ambaye yeye hakuwapo kwenye makabidhiano hayo.

No comments:

Post a Comment