Pages

Pages

Sunday, March 17, 2013

Kituko cha wiki: Chizi ageuka trafic maeneo ya Sinza Kijiweni

DUNIANI kuna mambo. Mtu huyu ambaye ni chizi, alikutwa juzi jioni maeneo ya Sinza Kijiweni akiongoza magari kwa staili ya aina yake. 

Awali alikuwa amekaa kando ya barabara akifanya fujo hasa kwa akina mama, lakini dakika mbili aliinuka na kuvamia barabara na kujifanya trafic. 

Hata hivyo, wapo waliomsikiliza kama unavyoona watu hao wamesimamisha magari yao, lakini aliposhindwa kuyaruhusu kwa dakika kadhaa wakati uwezekano wa kupita ulikuwapo, ndipo alipoibua hofu kwa wenye magari yao kuwa anaweza hata kupasua kioo ukizingatia kuwa mkononi alikuwa ameshika rungu.

Chizi huyo alizidi kuibua hofu hadi kijana mmoja alipojitoa mhanga na kumvamia na kumtoa barabarani, jambo ambalo liliwafanya madereva hao waendelee na safari zao. Watu wanashauriwa kuwa makini wanapokuwa kwenye vyombo vya usafiri. Picha na Kambi Mbwana

No comments:

Post a Comment