Pages

Pages

Sunday, March 03, 2013

CCM yawapiga msasa vijana Mbagala

 Katibu Kata wa UVCCM, Emmanuel John akiwakaribisha waalikwa wote wakae sawa kwa semina elekezi ya kiuongozi iliyofanyika kwa vijana wa Kata ya Mbagala. Pia alitumia wasaa huo kumkaribisha Mwenyekiti wa UVCCM wa kata ya Mbagala, Abdulhaman Ngamba afungua kikao.
 Mwenyekiti wa UVCCM, Kata ya Mbagala Ndg Abdulhaman Ngamba akifungua kikao cha semina elekezi kwa Vijana wa Kata ya Mbagala.
 Mgeni rasmi ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, Kata ya Mbagala Ndg Kassim Ngamba akibariki kuanza kwa shughuli husika ya Semina elekezi ya Kiuongozi kwa Vijana wa Kata ya Mbagala kwa ngazi ya Mashina, Matawi na Kata.



 Katibu Kata wa UVCCM, Ndg Emmanuel John akisoma taarifa fupi ya hali ya Umoja wa Vijana wa CCM kwa kata ya Mbagala pamoja na kuwaelezea malengo ya kufanyika kwa semina elekezi kwa Vijana iliyofanyika Jumamosi 02.03.2013
 Mwendesha Semina elekezi ambaye pia ni Katibu Uhamasishaji na Chipukizi wa Wilaya ya Temeke, Ndg Halfan Sabuni akitoa semina kwa vijana wa Kata ya Mbagala ili wajue wajibu na majukumu yao kiutendaji pamoja na kujua mipaka yao ya kazi.
 Baadhi ya Vijana waliohudhulia semina hiyo elekezi wakifuatilia kwa umakini Mkubwa kile kilichokuwa kikifundisha kwa kusikiliza na kusoma vitini walivyopewa.

 Meza kuu nayo pia ilikunwa na utolewaji wa semina hiyo elekezi.
 Mwendesha semina elekezi ambaye pia ni Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Ndg Halfani Sabuni akiendelea kutimiza majukumu yake huku Katibu wa Vijana Kata ya Mbagala. akimsikiliza kwa Umakini kubwa
  Katibu wa CCM wa Kata ya Mbagala, Ndg Isaya Tonga naye pia alikuwa mmoja wa wahudhuliaji wa semina hiyo ambapo alipata fursa ya kuwafunda vijana juu ya namna ya kuendesha shughuli za kisiasa kwa  Makatibu na namna gani ya kuwa Kijana mtiifu na shupavu wa UVCCM.

 Diwani wa Kata ya Mbagala, Aggrey Kayombo akichangia neno kwenye semina hiyo elekezi kwa vijana wa kata ya Mbagala
 Mjumbe wa Baraza la Mkoa wa DSM, Ndg Teddy akitoa msisitizo kwa vijana kuchapa kazi na wasiwe legelege.
Mwenyekiti wa UVCCM (W) Temeke, Ndg Oliver Mwambope ambaye naye pia alishiriki kukazia masuala mbalimbali yaliyozungumzwa kwenye semina hiyo.
Baadhi ya Wajumbe walioshiriki semina hiyo elekezi kwa Vijana wa Kata ya Mbagala.

No comments:

Post a Comment