Pages

Pages

Thursday, February 14, 2013

Utoaji wa vitambulisho vya Taifa upande wa Zanzibar awamu ya kwanza




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraz la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akikaribishwa na Mkurugenzi Mkuu wa vitambulisho vya Taifa,Dicson Maimu, alipowasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani, Nje ya Mji wa Zanzibar,katika Utoaji wa vitambulisho vya Taifa,awamu ya kwanza kwa upande wa Zanzibar.


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Devis Mwamunyange, akiweka kidole Gumba kufanya uhakiki katika mashine maalum, wakati wa Utoaji wa vitambulisho vya Taifa, awamu ya kwanza kwa upande wa Zanzibar, katika hafla iliyofanyika leo katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani, Nje ya Mji wa Zanzibar. Picha na Ramadhan Othman, Ikulu

No comments:

Post a Comment