Pages

Pages

Wednesday, February 06, 2013

Uchaguzi TAFCA, mmoja tu kuwania Mweka Hazina


Boniface Wambura, Msemaji wa TFF

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAKATI Uchaguzi wa Chama cha Makocha Tanzania (TAFCA), ukipangwa kufanyika Februari 14, mkoani Morogoro, hadi sasa nafasi ya Mweka Hazina ikiombwa na mwanamichezo mmoja tu, ambaye ni Jovin Ndimbo.

Mbali na Ndimbo, nafasi nyingine za uchaguzi huo zinawaniwa na Army Centimeya, Said Nasoro ambao wameomba kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa (TAFCA), Eugene Mwasamaki, alisema kwamba wadau wengine waliochukua fomu hizo ni Juma Chaponda, Juma Mpuya na Tifika Kambi wanayetaka nafasi ya Makamu Mwenyekiti.

Alisema nafasi ya Katibu Mkuu inaombwa na Abdallah Mitole, Charles Ndagala na Hamis Kisiwa, ambaye hawa watachuana kuitaka nafasi hiyo nyeti TACFA.

“Wengine ni Mjumbe wa Mkutano Mkuuiliyoombwa na Kamwaga Tambwe, huku nafasi kama hiyo kwa upande wa wanawake ikiombwa na Isabela Kapela, huku Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ikiombwa na Samson Mkotya,” alisema Mwasamaki.

Hapo kabla, uchaguzi wa TAFCA, ulisimamishwa na Kamati ya Uchaguzi kwa kutokidhi vigezo, hivyo kuwaondolea sifa ya kuingia kwenye Uchaguzi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), uliopangwa kufanyika Fabruari 24.

No comments:

Post a Comment