Pages

Pages

Saturday, February 09, 2013

Ruaha Marathon kufanyika Mei 25 mkoani Iringa


Mratibu wa Ruaha Marathon, Albert Sanga

Na Rahimu Kambi
SHIRIKA la Mindset Empowerment, waandaaji na waendeshaji wa mbio za kila mwaka ambazo ni za pili kwa ukubwa Barani Afrika za Ruaha Marathon; limesema kuwa mwaka huu mbio hizo zimepangwa kufanyika Mei 25, mkoani Iringa.

Mbio hizi zinashirikisha watu wa aina na rika zote wakiwemo walemavu kwa kukimbia kilomita, 3, 6, 21 na 41. 

Akizungumza kwa njia ya simu, Mratibu wa mbio hizo, Albert Sanga, alisema kuwa jumla ya washiriki na wageni (2,000) watakuwapo kwenye mashindano hayo.

Alisema wanatarajia kufanya mashindano yenye mguso kwa mkoa wao wa Iringa, huku wakiamini pia watu kutoka nje ya nchi watashiriki.

Watu kutoka Mataifa mbalimbali duniani, walihudhuria mashindano haya mwaka jana, hivyo mwaka huu tunatarajia kupokea washiriki na wageni wengi zaidi. 

"Tumeshaanza kuandikisha washiriki tangu Desemba, 2012, hivyo natumia fursa hii kuwaalika watu kujiandikisha sasa ili waweze kushiriki mbio hizi zenye mguso," alisema Sanga.

Aidha waandaaji wa mbio hizo wameweka utaratibu wa kujiandikisha kwa njia ya mtandao, (online registration) kwa kupitia www.ruahamarathon.com au kwa namba +255719 127 901.

No comments:

Post a Comment