Pages

Pages

Wednesday, February 13, 2013

Nyota wa Wanaume Halisi afariki Dunia

Marehemu Baraka Seleka (katikati), enzi za uhai wake.
 
MSANII wa kundi la TMK Wanaume Halisi Baraka Seleka maarufu kama BK amefariki dunia katika hospital ya Muhimbili kutokana na maradhi ya tumbo yaliyokuwa yakimsumbua.

Hayo yalibainishwa na mmoja wa wasanii wa kundi hilo, Rich-One alipokuwa akizungumzia kifo cha msanii mwenzao aliyefariki leo saa 11 alfajiri.
 
Rich-One amesema taratibu za mazishi zitatolewa hapo baadae baada ya kufanya utaratibu wa kuzungumza na familia yake. Mwimbaji huyo ni kati ya wale waliokuwa wakiipaisha zaidi kundi lao, huku akifariki kwa maradhi ya tumbo.

No comments:

Post a Comment