Pages

Pages

Wednesday, February 13, 2013

Francis Cheka kutandikana na Thomas Mashali

          Francis Cheka (kushoto) akiwa na Adam Tanaka (katikatia) na Thomas Mashali (kulia)

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Ngumi la Kimataifa Afrika (IBF/Africa), limetoa kibali kwa bondia Francis Cheka ambaye ni bingwa wa Africa katika uzito wa Super Middle kutetea ubingwa wake dhidi ya bondia Thomas Mashali wa Tanzania, likipangwa kufanyika Mei Mosi, katika Ukumbi wa PTA, jijini Dar es Salaam.

Mabondia hao wawili walikutana jana     Februari 13 katika hoteli ya Ndekha, iliyoko Magomeni Kondoa na kutia sahihi mkataba wa kupigana kwenye pambano hilo.

Taarifa iliyotumwa na Rais wa Shirikisho hilo, Onesmo Ngowi, ilisema kuwa Mashali ambaye ndiye bingwa wa Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBF) katika uzito wa Middle ana kiwango kizuri cha kushindana na Cheka katika pambalo hilo.

Ilisema kuwa itakuwa mara ya pili kwa bondia Francis Cheka kutetea mkanda alioushinda Aprili 29, mwaka 2012 dhidi ya bondia machachari Mada Maugo wa Tanzania.

“Cheka aliutetea vyema mkanda wa ubingwa wa IBF/Africa dhidi ya bondia Chiotcha Chimwemwe ambaye ni Afisa katika jeshi la Malawi siku ya Boxing Day (26 Decewmber 2012) katika jiji la Arusha.

“Kama Francis Cheka atashinda tena pambano hili, atapewa nafasi ya kupigana kugombea mkanda wa IBF wa mabara (IBF I/C),” ilisema taarifa hiyo.

Pambano hili linaandaliwa na kampuni ya Mumask Investment and Gebby Pressure ya jijini Dar es Salaam chini ya uratibu wa Adam Tanaka.

No comments:

Post a Comment