Pages

Pages

Tuesday, February 19, 2013

Nyosh wa Wazee wa Ngwasuma awapayukia wanamuziki Bongo



Rais wa FM Academia, Nyosh el Sadaat

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
RAIS wa bendi ya FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma, Nyosh el Sadaat, amesema mwanamuziki ambaye hana nidhamu hawezi kuwa na mafanikio katika maisha yake ya sanaa.

Akizungumza mwishoni mwa wiki katika onyesho lao la kila Jumapili katika Ukumbi wa New Msasani Club, Nyosh alisema kwamba kwa sababu hiyo, ipo haja ya wanamuziki kujifundisha nidhamu.

Alisema hata katika baadhi ya shoo, mwanamuziki mwenye nidhamu anakuwa nyuma ya jukwaa na sio kuzurula ovyo ovyo kiasi cha kushindwa kujipanga anapohitajika jukwaani.

“Jamani hatuwezi kufanikiwa katika maisha ya muziki kama nidhamu zetu ni ndogo, hivyo naomba sisi ambaye tunaishi kwa kazi hii tujifunze jambo hilo maana ni muhimu mno.

“Nasikitika kuona wanamuziki wangu, wakiwamo marepa wanazagaa tu wakati wanastahili kutulia nyuma ya jukwaa kwa pamoja, maana hii ni kazi na lazima tuiheshimu,” alisema Nyosh.

Maneno ya Nyosh yalitokana na kuwapandisha wanamuziki wake mmoja baada ya mwingine kuonyesha uwezo wao, hasa kwa nafasi za marepa ambazo kwa Wazee hao wa Ngwasuma, kumekuwa na ushindani wa aina yake na kuleta burudani za aina yake.

No comments:

Post a Comment