Pages

Pages

Tuesday, February 12, 2013

Mwimbaji wa Injili sasa ahamia kwenye soko la filamu, vitabu


Mwimbaji wa Inji, Dorice Mkangama

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa nyimbo wa Injili, Dorice Mkangama ambaye kwa sasa anakamilisha albamu ya tano, amesema kuwa pia yuko mbioni kufyatua filamu sita kwa mpigo ambazo sasa anaendelea kuziandaa.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, huyo alizitaja filamu hizo kuwa ni 'Karama ya Almasi', 'Money Kingdom', 'Lango la Giza', 'The Dream', 'The Singer' na 'The Prophetic Sin'.

"Mimi ndiye mtayarishaji na muongozaji huku kazi hii ikinichukua muda mrefu na sasa niko kwenye hatua za mwisho kukamilisha filamu hizo," alisema Mkangama na kuendelea:

"Ninamshukuru Mungu kwa sababu amejalia vipaji vingi tu ambavyo ni muhimu nivitumie kwa kazi yake, ndiyo maana ninaimba na pia nina uwezo wa kutunga vitabu," alisema.

Alisema katika kutumia vipaji vyake hivyo, anajiandaa pia kutoa vitabu
kadhaa vikiwemo vya 'King'amuzi cha Ndoto', 'Miujiza', 'Mjue Adui Yako', 'Upako' na 'Jinsi ya Kujifungua Katika Vifungo'.

Alisema kuwa ana kazi kazi tatu ambazo ni za kuandaa filamu, utunzi wa vitabu na pia kukamilisha albamu mbili kwa mpigo za  Namngoja Bwana na Mvua ya Baraka.

Mkangama alijitosa kwenye muziki wa Injili tangu mwaka 2005 akiwa na albamu ya  kwanza ya 'Tazama Bwana' kisha ikafuatia ya pili iitwayo 'Yesu Namba Moja', 'Mikononi mwa Yesu' na sasa anaandaa mbili kwa mpigo.

No comments:

Post a Comment