Pages

Pages

Monday, February 11, 2013

Machafuko ya Waislamu, Wakristo na hoja ya kuchinja yaikera CCM, wilayani Mbogwe



Picha hii imewekwa kama sehemu ya kumuwakilisha Katibu wa CCM, wilayani Mbogwe, Augustine Mbogo, ambaye picha yake tunafanya mpango wa kuipata.

Na Mwandishi Wetu, Geita
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kwa kupitia Katibu wake wa wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita, imewajia juu baadhi ya wanasiasa kutoka Upinzani, kwa madai kuwa wameanzisha hoja ya kuchinja inayoendelea kuitafuna nchi kwa sasa, hasa kwa leo kutokea machafuko wilayani Chato, mkoani humo.

Hayo yamesemwa na Katibu wake, Augustine Mbogo, ikiwa ni saa chache baada ya kuripotiwa machafuko yaliyozuka leo, huku kadhia hiyo ikisababishwa na hoja ya kuchinja.

Akizungumza na Handeni Kwetu, Mbogo alisema kwamba tangu mwanzo Waislamu walikuwa ndio wachinjaji kwa ajili ya kuleta maisha ya ushirikiano kwa jamii za Kikristo na Kiislamu.

Alisema kadri siasa za maji taka zilipoanzishwa na wanasiasa wanaotaka kuiweka nchi kubaya, hoja hiyo ilianza kufanyiwa kazi, ikiwa ni jambo lisilokubaliwa hata kidogo.

“Mimi ni kiongozi wa CCM wilaya, lakini pia ni jamii ya Roman Catholic, nikikuwa huku nashuhudia hata Mapadre wanavyoita jamii ya Kiislamu kwa ajili ya kuchinja, hivyo naiomba serikali kuifanyia kazi haraka tatizo hili linaloweza kuwagawa Watanzania na kuleta machafuko zaidi.

“Sasa leo imeibuliwa hoja hiyo na watu ambao siku zote wanataka kuiweka Tanzania katika hatari, ndio maana kila mahali wanajaribu kuingia, ikiwamo Ukabila, udini na nyinginezo,” alisema.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu wilayani Chato, mkoani Geita, kumetokea machafuko, baada ya Wachungaji wa AIC kutenga eneo la Buselesele kwa ajili ya machinjio ya Wakristo wao, maeneo ya Katoro.
Taarifa zaidi zitaendelea kukujia kwa kufanya mawasiliano na wadau wetu waliokuwapo mkoani Geita.
Handeni Kwetu inapinga vikali machafuko hayo ya kidini kwa hoja ya kuchinja, ambayo tangu Uhuru, haijawahi kuwagawa Watanzania.

1 comment:

  1. HII NI HATARI! Tanzania imekuwapo na wazee wetu wameishi kwa amani na hata ubaguzi huu wa kidini na kuchinja walitambua na kuheshimu dini na maagizo yake. Mimi nikiwa mmoja wao nimeishi na ndugu waislamu lakini kwa kuheshimu tumekuwa tukichinjiwa na wao ili kudumisha udugu wetu. Hii kwetu Tanzania imekuwa kama sheria zetu za kimila kwani sio lazima ziandikwe popote. Leo hiki kinatoka wapi? Siasa za majitaka zitatumaliza, Laana ya mwalimu Nyerere aliyosema tukianza kubaguana kwa misingi ya dini/kabila/ maeneo yetu basi haitaishia hapo tutamalizana. Utabiri unatimia. Eee Mungu wanaotufikisha huko waangamize na malengo yao yasitimie.

    ReplyDelete